Headlines News :
Home » » YOUNG DEE KUIBUKA NA KITU 'KIJUKUU'

YOUNG DEE KUIBUKA NA KITU 'KIJUKUU'

Written By Bashir Nkoromo on Tuesday, July 30, 2013 | 11:01 AM


Na Elizabeth John
MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Young Dee anajipanga kuachia kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Kijukuu’ ikiwa ni muendelezo wa kuwashika mashabiki wa kazi zake.

Young Dee alishawahi kutamba na kazi ya ‘Dada anaolewa’ licha ya kuwa na kazi nyingi ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika tasnia ya muziki huo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Young Dee alisema kazi hiyo kaitengeneza katika studio ya MJ rekodi chini ya mtayarishaji wake mahiri, Marco Chali.

Pia aliwataka wapenzi wa kazi zake wakae mkao wa kula kwaajili ya kazi hiyo ambayo anaamini itafanya vizuri kutokana na mashairi yaliyomo ndani yake kubeba ujumbe katika jamnii.

“Naomba wapenzi wa kazi zangu wake mkao wa kula kwaajili yakuipokea kazi hii, naimani nitaisambaza hivi karibuni ikiwa ni pamoja na video yake ili niwape burudani iliyokamilika wapenzi wa kazi zangu,” alisema.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Google+ Followers

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo Blog: SPORTS PAGE - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template