Headlines News :
Home » » FFU WA NGOMA AFRICA BAND KUSHEREHEKEA MIAKA 20 NDANI YA INTERNATIONAL AFRICAN FESTIVAL TUBINGEN, UJERUMANI

FFU WA NGOMA AFRICA BAND KUSHEREHEKEA MIAKA 20 NDANI YA INTERNATIONAL AFRICAN FESTIVAL TUBINGEN, UJERUMANI

Written By Bashir Nkoromo on Sunday, August 4, 2013 | 2:56 AM

KAMANDA RAS MAKUNJA
Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa Band" a.k.a FFU
yenye makao yake nchini ujerumani.Muzimu huo wa muziki "Ngoma Africa band,utasherekea miaka 20 tangu ianzishwe mwaka 1993 na kiongozi wake 
mwanamuziki Ebrahim Makunja almaarufu kamanda Ras Makunja wa FFU.

Bendi hiyo yenye wapenzi,washabiki na wadau lukuki katika kila kona duniani
itasherekea miaka 20 ndani ya International African Festival Tubingen 2013,katika
viwanja vya Fest-platz huko Tubingen,Ujerumani,ambapo wapenzi wa bendi hiyo
wapewa siku mbili kuanzia tarehe 9 na 10.08.2013 kupata burudani ya bendi hiyo.

Ngoma Africa Band a.k.a FFU imetajwa kuwa ndio bendi ya kiafrika hiliyoweza kudumu kwa muda mrefu katika medani ya muziki barani ulaya,na kuweza kujizolea wapenzi na washabiki katika kila kona.

Washabiki na wadau wa bendi hiyo ndio wanao jigamba kuwa wanamiliki na
kuipa nguvu bendi hiyo na kiongozi wa bendi hiyo Ras Makunja na wanamuziki
wa bendi ni watumishi tu wanao watumikia washabiki na wapenzi wa Ngoma Africa.
Tunaitakia kila la heri Ngoma Africa band tusikose kuwasikiliza FFU at
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo SPORTS - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template