Na Jennifer Chamila-MAELEZO
KIJANA wa Kitanzania Hamisi Kondo aibuka mshindi wa dunia
katika mashindano ya kuruka kamba yaliyo fanyika Orland Marekani Julia 5 hadi
Julai 13 mwaka huu.
Mashindano hayo yalihusisha
nchi kumi na nne zikiwa na wachezaji 480 huku Bara la Afrika likiwakilishwa na Tanzania,
Kenya na Afrika ya Kusini ambapo kijana Hamisi mwenye
umri wa miaka 14 Mtanzania aliweza kujinyakulia ushindi huo.
Kijana huyo ambaye ni yatima aliyelelewa na kituo cha
kulelea watoto yatima cha Dogodogo Center kilichopo jijini Dar es Salaam na kupata
mafunzo ya mchezo wa kuruka kamba kituoni hapo na
baadae kupata ufadhili kutoka kwa Bwana
na Bibi Amy Canady nchini Marekani ambako aliweza
kusoma na kuendeleza kipaji chake.
Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Hamisi amezungumzia mafanikio yake na kuwaasa
vijana wenzake kutokata tamaa ya maisha
kwa kuwa na juhudi ya kupambana ili waweze kufikia malengo waliyojiwekea.
“Nawaomba watoto wa mtaani na yatima kutokata tamaa ya
maisha kwani hata mimi nilikuwa kama wao na nimeweza kufanya juhudi na kufanikiwa”alisema
Hamisi.
Naye Mkurugenzi Msaidizi
wa Idara ya Maendeleo ya Michezo ,kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Bi. Juliana Yassoda aliwaomba
vijana kutong’ang’ania michezo mikubwa kama mpira wa miguu kwani kuna michezo midogo
midogo ambayo wanaweza kucheza na kufanikiwa kama ilivyo kuwa kwa Hamisi.
Pia Mwenyekiti wa Kituo cha Kufundisha Michezo Tanzania (TSTC),
Bw.Dennis Makoi ambaye alishirikiana na kituo cha dogodogo kumtafutia ufadhili
Hamisi nchini Marekani,ametoa shukrani zake za dhati kwa familia ya Bw. na
Bi.Amy Canady wa huko Marekana kwa
ufadhili na kusaidia kufanikisha ushindi
huo. Hivi sasa Hamisi
anaendelea na masomo nchini Marekani.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !