Waziri
wa habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dr Fenela Mukangara (kulia) akimkabidhi
Bendera ya Taifa Mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Urembo ya Dunia, Redd's Miss Tanzania Briggiter Wilfred kulia ikiwa ni ishara ya
kutambua wajibu wake kwa kipindi chote cha mashindano hayo nchini
Indobesia, Kushoto ni Mkurugenzi wa LINO AGENCY Hashim Lundenga.
Na Mwandishi Wetu
REDD’S Miss
Tanzania, Brigitte Alfred amedai atahakikisha anatwaa taji la dunia (Miss
World), ambalo litafanyika Septemba 28 huko Indonesia.
Akizungumza
wakati akiagwa katika hafla iliyofanyika kwenye hoteli ya Giraffe iliyopo
Kunduchi, Dar es Salaam, Brigitte alisema nia yake kubwa ni kushindana na si
kuwa msindikizaji.
“Nina uhakika
mkubwa wa kutwaa taji hilo, kwani vigezo vyote ninavyo na nimejiandaa kwa muda
mrefu mno,” alisema Brigitte.
Mrembo huyo
ambaye anatarajiwa kuondoka Jumatatu kwenda Indonesia alisema, Kamati ya Miss
Tanzania imemsaidia kwa kiasi kikubwa, hivyo ni matarajio yake atatwaa taji
hilo.
“Niseme wazi
nimejiandaa kwa muda mrefu mno na nashukuru wote walionisaidia kwa njia moja au
nyingine na hii inanipa moyo wa kufanya vizuri zaidi,” alisema.
Naye Waziri wa
Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenella Mukangara aliyekuwa mgeni
rasmi, wakati akimkabidhi bendera ya taifa alimtaka ahakikishe anaipeperusha
vizuri na kufanya vyema katika mashindano hayo.
“Fahamu fika
kwamba unakwenda Indonesia kama Miss Tanzania na si Brigitte, hivyo
unatuwakilisha Watanzania wote, sisi tuko nyuma yako unachotakiwa ni kujiamini
tu na utafanikiwa.”
Mrembo huyo
alifanikiwa kulitwaa taji la Redd’s Miss Tanzania mwishoni mwa mwaka jana,
akitokea kitongoji cha Sinza na Kanda ya Kinondoni.
Redd’s Miss
Tanzania kwa sasa inadhaminiwa na kinywaji cha Redd’s Original kinachozalishwa
na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !