Headlines News :
Home » » BASATA YATOA USHAURI KWA WASANII

BASATA YATOA USHAURI KWA WASANII

Written By Bashir Nkoromo on Thursday, February 6, 2014 | 1:50 AM

Na Peter Mwenda, Mkuranga

MWENYEKITI wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Profesa Penina Mlama ametoa wito kwa wasanii kuchangamkia kuchangia ujenzi wa nyumba unaratibiwa na Mtandao wa wasanii Tanzania (SHIWATA) ili kujiandalia makazi.


Akizungumza baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa nyumba za wasanii katika kijiji cha Mwanzega, wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani, Profesa Mlama alisema makazi ni sehemu ya maisha ya binadamu hivyo wasidharau mradi huo ni faida kubwa kwao.



Alisema nyumba ambazo ameziona ni nzuri, imara na zinauzwa bei ya chini ambayo huwezi kuzipata sehemu nyingine yoyote nchini Tanzania na kuongeza kuwa kujenga kwa lengo la kuishi pamoja kunatoa fursa ya wasanii kubuni njia nyingine ya kuanzisha miradi mbalimbali.



Profesa Mlama alitaka SHIWATA isikate tamaa bali iendelee kuwashawishi wasanii wajiunge na kuchangia ujenzi wa nyumba ili baadaye wasitafute visingizio kuwa hawakupewa fursa hiyo.



Naye Katibu Mtendaji wa BASATA,Godfrey Mngereza alisifu SHIWATA kubuni njia ya kuwasainia wasanii kupata makazi na kuahidi kuwa baraza hilo litatoa ushirikiano na kutoa ushauri kila unapohitajika.



Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema mpango wa ujenzi wa nyumba za wasanii utaendelea kote nchini na kuwataka wasanii waungane kufanya kazi zao kwa pamoja.



Alisema mpaka sasa nyumba 38 zimekabidhiwa kwa wasanii waliochangia ujenzi katika kijiji cha Mwanzega Mkuranga na nyingine 21 zinatarajiwa kukabidhiwa Machi mwaka huu.



SHIWATA mbali ya kusimamia ujenzi wa nyumba za wasanii inasimamia matamasha ya wasanii wachanga (Underground) kuendesha makongamano ya kupambana na kuzuia dawa za kulevya na kutoa elimu na maadili kwa wasanii.

 Mwenyekiti wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Profesa Penina Mlama akikagua nyumba za wasanii katika kijiji cha Mwanzega, Mkuranga jana, kulia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA),Cassim Taalib na Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza.
 Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA),Godfrey Mngereza akizungumza katika moja ya nyumba zinazojengwa na Mtandao wa wasanii Tanzania (SHIWATA) kulia ni Mwenyekiti wa BASATA, Profesa Penina Mlama.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo SPORTS - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template