Headlines News :
Home » » UCHAGUZI TASWA WAPIGWA KALENDA, SASA KUFANYIKA MACHI 2 BADALA YA TAREHE 16 MWEZI HUU ILIYOKUWA IMEPANGWA

UCHAGUZI TASWA WAPIGWA KALENDA, SASA KUFANYIKA MACHI 2 BADALA YA TAREHE 16 MWEZI HUU ILIYOKUWA IMEPANGWA

Written By Bashir Nkoromo on Friday, February 7, 2014 | 8:39 AM

UCHAGUZI Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), uliokuwa umepangwa kufanyika Februari 16 umesogezwa mbele kwa wiki mbili na sasa utafanyika Machi 2, mwaka huu jijini Dar es Salaam.
 
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando (Pichani), imesema uamuzi wa kusogeza mbele tarehe ya kufanyika uchaguzi huo imechukuliwa na Sekretarieti ya TASWA kutokana na sababu mbalimbali, lakini kubwa ni kutoa nafasi kwa wanachama wengi zaidi kulipia ada zao kwa ajili ya kushiriki mkutano huo wa uchaguzi.
 
Hadi kufikia leo mchana idadi ya wanachama waliokuwa wamelipia ada ni 57 kati ya wanachama karibu 150 waliopo katika leja na kati ya waliolipa ni wanne tu ndiyo wamelipia ada ya miaka mitatu kama walivyotakiwa wakati waliobaki wamelipia mwaka mmoja.
 
Kumekuwa na changamoto mbalimbali zimejitokeza katika suala hili la kulipia ada, ikiwa ni pamoja na maombi ya baadhi ya wanachama walipie mwaka mmoja na kisha ada nyingine chama kiwawekee utaratibu wa kulipa siku za usoni kadri itakavyoonekana inafaa.
 
Kutokana na hali hiyo sekretarieti ya TASWA imepokea maombi hayo na kwa vile uamuzi huo ulifikiwa na kikao cha Kamati ya Utendaji ya TASWA, itayawasilisha kwenye kikao kama hicho kitakachofanyika Jumatatu Februari 17 kujadili masuala mbalimbali yahusiyo mkutano huo, ikiwa ni pamoja na kupitia orodha ya wanachama wanaostahili kushiriki mkutano wa uchaguzi.
 
Hatua ya awali ambayo imefanyika ni kusogeza mbele tarehe ya mwisho ya kulipia ada, ambayo awali ilikuwa Februari 4 na sasa itakuwa Februari 15 mwaka huu saa kumi alasiri na hakutakuwa na muda wa ziada.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo SPORTS - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template