Mtanzania mmoja kati ya wawili walioshirikishwa katika filamu ya “Woman with Altitude” iliyoandaliwa na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Ashura Kayupayupa (kulia), akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye hoteli ya Doubletree by Hilton Zanzibar. Kushoto ni Mratibu wa Majaji wa tuzo za ZIFF 2014, Fabrizio Colombo na Katikati ni Afisa Habari wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Fizza Moloo.(Picha na Zainul Mzige wa MOblog).
Na Beda Msimbe, Zanzibar
UNAWEZA kudhani kamba kila aliyefanikiwa amezaliwa na kijiko cha fedha, yaani amezaliwa katika eneo lenye hali shwari na kitanda chake ni mayai ya dhahabu, kumbe sivyo kabisa.
Hili linajadliwa kwa undani katika sinema iliyoandaliwa na Shirika la Mpango wa chakula duniani (WFP), Women with Atitude.
Sinema hii ambayo inaoneshwa katika ukumbi wa wazi wa Ngome Kongwe imetengenezwa na watanzania kwa ajili ya kuhamasisha Watanzania kutambua kwamba maisha ni mkusanyiko wa utatuzi wa migogoro inayowakuta na kwa kupitia elimu.
Women with Altitude inazunguka katika vitu vingi, lakini cha maana ni wanawake wanaojiamini.
Baada ya kufanikiwa kupanda mlima Everest mwaka 2008, wanawake saba wa Nepal waliamua kupanda milima mingine mirefu katika mabara mbalimbali wakiwa na lengo la kutoa ushawishi kwa wanawake na wasichana duniani kote kufuatilia mambo ambayo yanaonekana ni magumu na hayawezekani.
Machi 2013,wanawake hao walipata ushosti kutoka kwa wanawake wa Kiafrika wane akiwemo muigizaji wa Afrika kusini Hlubi Mboya,ambaye anatambulika sana kwa kuigiza nafasi ya mtu anayeishi na VVU kama Nandipha kwenye Isidingo kupanda mlima mlima mkubwa wa bara la Afrika, Mlima Kilimanjaro.
Afisa Habari wa WFP, Fizza Moloo akizungumzia kuhusiana na filamu iliyopewa jina la “Women with Altitude” ambapo ndani yake wameshirikishwa wasichana wa kitanzania wawili na imefadhiliwa na shirika hilo imeonyeshwa jana ndani ya viunga vya Ngome Kongwe visiwani Zanzibar linakoendelea tamasha la 17 la ZIFF 2014.
Tofauti ya utamaduni na mazingira kwa wanawake wote 11 ilikuwa pia ni ishara ya matatizo waliyokumbana nayo katika maisha yao.
Filamu hii ya Women with attitude inaonesha matatizo ya wanawake hao 11 waliokuwa wakikumbana nayo katika maisha yao yote, na nafasi ya elimu katika kuwasaidia kufika pale walipo kwa leo.
Wanawake hawa wanaonekana wakikabiliana na Mlima Kilimanjaro, wakiangalia maisha ya wenzao na kuwashawishi katika kutokata tama na badala yake kutumia changamoto kuleta maisha yenye hadhi ya aina yake.
Ofisa habari wa WFP, Fizza Moloo akizungumza katika mahojiano alisema kwamba taarifa iliyomo ndani ya sinema hiyo ni ujumbe tosha kwa vijana na wanawake kuhusu ukweli wa maisha na namna ya kuyabadili.
Baadhi ya waandishi wa habari, waigizaji wa filamu na Producers waliohudhuria mkutano huo ndani ya hoteli ya Doubletree by Hilton.
Mmoja wa washiriki wa sinema hiyo kutoka tanzania, Ashura Kayupayupa alisema kwamba alipoteza baba yake akiwa na umri wa miaka minane, lakini mafanikio yake yote yametegemea jinsi alivyokabiliana na shida zilizopo.
Baba yake alikufa kwa ajali ya gari.
Alisema baada ya baba yake kufa hali ilikuwa mbaya katika familia kwa kuwa mama yake alikuwa anamtegemea baba yake kwa kila kitu, wakajikuta hawana namna ya kufanya.
Ashura ambaye amezaliwa miaka 24 iliyopita anasema kwamba kutokana na vikwazo ambavyo amekumbana navyo toka baba yake kuondoka vilimfanya kuwa na mawazo mengine ya maisha.
Alisema baada ya baba yake kufa alienda kulelewa na ndugu wa baba yake ambao walikuwa wanamvuruga na kumtesa.
Ashura Kayupayupa akibadilishana mawazo na mbunifu wa mavazi mkongwe Farouk Abdallah mara baada ya mkutano na waandishi wa habari.
Alisema licha ya kuteswa alikuwa anaenda shule kama kawaida na kujitahidi kusoma.Amesoma shule ya msingi Temeke, kisha sekondari ya Kijitonyama kabla ya kuenda al Haramain kumaliza kidato cha sita na kwenda Chuo Kikuu cha Tumaini kuchukua sheria.
Kwa sasa yeye ni mwanasheria na anasema kwamba kuacha kusoma kwa sababu ya kuteswa ni upuuzi kwani ndio zinaua fursa ya kujitambua duniani na kujiendeleza.
Alisema ni vyema wanawake wasikimbilie kulalamika kwamba hawakusoma kwa sababu ya mateso au wazazi wao kufa. Alisema ni vyema mtu kuwa na malengo na kujifunza vitu hata kwa kujitolea mpaka kieleweke.
Ashura Kayupayupa akipiga picha ya kumbukumbu na mbunifu wa mavazi visiwani Zanzibar Farouk Abdallah.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !