Uongozi
wa Klabu ya Young Africans umeshangazwa na taarifa zilizoandikwa kwenye
mojawapo ya vyombo vya habari juu ya Wanachama wa Tawi la Tandale
kusema hawatambui kufutwa kwa Tawi lao ni za Ubabaishaji.
Mnamo
Mei 04, 2014 Mwenyekiti wa Klabu ya Young Africans Bw Yusuf Manji
alitangaza kulifuta Tawi la Tandale kutokana na kua chanzo cha migogoro
ndani ya klabu kwa kipindi cha mrefu, ili hali likiwa halina hadhi ya
kuwa Tawi Kamili.
Kufutwa
kwa Tawi la Tandale kunatokana na kutotimiza idadi ya wanachama mia
moja (100) kama inavyojieleza kwenye Katiba ya Yanga SC, Ibara ya 6,
kipengele cha 4 "Kutakuwa na uundaji wa matawi katika maeneo mbalimbali
hapa nchini na nje ya nchi. Kiwango cha chini ya idadi ya wanachama
ambao wanaweza kunda tawi kisipungue watu mia moja (100)".
Ibara
ya 13, kipengele cha 2 kinasema " Kutolipa ada zake za uanachama kwa
muda wa miezi sita mfululizo bila ya sababu maalum inayokubalika na
Kamati ya Utendaji"
Baadhi
ya Wanachama walijifuta uanchama wao kutokana na kushindwa kulipia ada
zao za uanachana kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita, kama inavyojieleza
kwenye Katiba kwamba mwanachama asipolipia ada yake zaidi ya miezi sita
moja kwa moja anajifuta uanachama wake.
Hivyo
Uongozi wa klabu ya Yanga SC unaomba Umma na Wanachama wake Duniani
kote watambue kuwa Tawi la Tandale lilifutwa kwa kutokana na kutokidhi
vigezo, huku wanachama wake wengine watano wakijifuta uanachama kwa
kushindwa kulipia ada zao kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita.
Mwisho
wanachama wa klabu ya Yanga SC wanaombwa kulipia ada zao za uanchama
mapema kabla ya muda wao kumalizika ili waweze kushiriki mkutano mkuu wa
marekebisho ya Katiba utakaofanyika kwenye Ukumbi wa Bwalo la Polisi -
Oysterbay Juni Mosi 2014.
Beno Njovu
Katibu Mkuu - Yanga SC
Mei 23, 2014
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !