Headlines News :
Home » » SAMATA KUPEWA ENEO LAKE MWEZI UJAO

SAMATA KUPEWA ENEO LAKE MWEZI UJAO

Written By Bashir Nkoromo on Monday, May 23, 2016 | 2:54 AM

Na Mwandishi Wetu
MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umesogeza mbele kwa siku moja sherehe za kumkabidhi eneo mchezaji bora wa Afrika, Mbwana Samatta hadi Juni 5, 2016 ili kupisha pambano kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na timu ya Taifa ya Misri.
Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassima Taalib alisema jana Dar es Salaam kuwa  maandalizi ya sherehe hizo ambazo awali zilipangwa kufanyika Juni 4, 2016 yamekamilika na Mbwana atakabidhiwa hekari tano za eneo ambazo atalitumia kujenga Kituo cha wanamichezo katika eneo la Mwanzega, Mkuranga mkoa wa Pwani.
Alisema hivi karibuni baba mzazi wa mchezaji huyo, Mzee Ali Samatta alishukuru SHIWATA kutambua mchango wa mwanae katika medani ya soka nchini na kuahidi kusaidia kusimamia juhudi za mwanae katika kuendeleza michezo nchini.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Salum Madadi alithibitisha kufanyika mchezo wa Stars na Misri siku ambayo awali ilipangwa Mbwana kukabidhiwa eneo hilo.
Samatta anayecheza soka ya kulipwa Ulaya atatumia mapumziko ya mechi ya Stars na Misri kukabidhiwa eneo hilo na kadi ya uanachama wa SHIWATA katika kutambua mchango wake kuitangaza Tanzania kuwa mchezaji bora Afrika kati ya wachezaji wanaocheza mpira wa kulipwa ndani ya bara la Afrika.
Katika sherehe hizo wasanii 35 watakabidhiwa nyumba zao kati hiyo, wanachama watatu watakabidhiwa nyumba ndogo, 31 watakabidhiwa misingi na nyumba kubwa moja na kufikia idadi ya nyumba 185 ambazo zimekwisha jengwa kijijini hapo mpaka sasa.
Akizungumza katika mkutano wa wanachama kujiandaa na sherehe hizo walimuomba Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Mnauye awe mgeni rasmi ambapo pia waliomba dua la kumuombea Rais John Pombe Magufuli katika juhudi zake za kupambana na wabadhirifu wa mali ya umma.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Google+ Followers

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo Blog: SPORTS PAGE - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template