Headlines News :
Home » » SBL YAZINDUA SHINDANO LA WAPIGA MZIKI (DJ) “MIX MASTER” ITAKAYOSHIRIKISHA MIKOA MITANO

SBL YAZINDUA SHINDANO LA WAPIGA MZIKI (DJ) “MIX MASTER” ITAKAYOSHIRIKISHA MIKOA MITANO

Written By Bashir Nkoromo on Sunday, October 9, 2016 | 9:21 AM

Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo imetangaza kuzindua shindano la DJ bora ambalo linalenga  kuibua na kukuza vipaji katika sekta ya muziki na burudani nchini Tanzania.

Akizungumza wakati wa  uzinduzi wa shindano hilo jijini Dar es Salaam, Mkrugenzi wa Mawasiliano wa Serengeti John Wanyancha alisema kuwa  shindano hilo limedhaminiwa na  bia inayozalishwa na kampuni hiyo Smirnof Black Ice, na wakati huo huo  ikimaanisha kuwapatia mashabiki wa muziki  fursa ya kufurahia  vibao vya muziki vya hivi karibuni vitakavyochezeshwa na ma-DJ walio na vipaji vikubwa.

 Kwa mujibu wa Wanyancha, Smirnof Black Ice ni chapa inayoongoza  katika vighezo vya bia iliyotayari kunyweka ikiwa ni maarufu mioongoni mwa wanywaji wa tabaka la kati katika maeneo yote ya mjini na vijijini.

 “Tunaamini kwamba kupitia shindano hili SBL itawapa wakati mzuri  wapenzi wa muziki watakaokuwa wanatembelera baa  wakati tukitoa fursa maridhawa ya kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji katika ulimwengu wa muziki na ma-DJ.

Mkurugenzi huyo aliyataja majiji ambayo yatakuwa wenyeji wa matukio na idadi ya ma-DJ watakaotoa burudani  katika mabaa kwenye mabano kuwa ni Dar es Salaam (20), Dodoma (4), Arusha (5), Morogoro (4), na Mwanza (5). Shindani hilo linaanza mwezi huu wa Oktoba na  litadumu hadi Desemba.

Aidha Mkurugenzi huyo alisema kuwa hadhira inayolengwa katika  mashindano hayo ni  vijana walio na umri kati ya miaka 18 hadi 30 na kufafanua kuwa burudani hiyo inawafaa sana  wanafunzi wa vyuo vikuu na vyuo vingine vya elimu ya juu pamoja na vija walio na weledi.

“Itakuwepo zawadi nono kwa ma-DJ watakaoshinda,” alisema na kubainisha kwamba zawadi hizo zitajumuisha seti ya vifaa vya kuchanganya muziki, kompyuta mpakato na mashine kuchanganya muziki kwa washindi watatu watakaoingia fainali.

 “Tunatoa wito kwa ma-DJ wote, wasimamizi wa baa na wapenzi wa muziki katika majiji haya  kushiriki kwa wingi katika shindano hili la kuvutia  ili kufurahia na  burudani inayotolewa na sekta ya muziki nchini Tanzania,” alisema Wanyancha.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Google+ Followers

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo Blog: SPORTS PAGE - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template