Headlines News :
Home » » KIMOBITEL ATAMBULISHWA RASMI EXTRA BONGO NDANI YA WHITE HOUSE NA MEEDA SINZA USIKU WA KUAMKIA LEO.

KIMOBITEL ATAMBULISHWA RASMI EXTRA BONGO NDANI YA WHITE HOUSE NA MEEDA SINZA USIKU WA KUAMKIA LEO.

Written By Bashir Nkoromo on Sunday, September 16, 2012 | 11:22 AM

Khadija Mnoga aka KIMOBITEL akiimba wimbo wake mpya "Mgeni" wakati wa utambulisho wake rasmi wa kujiunga na Bendi ya Extra Bongo ndani ya New White House Kimara Korogwe Dar es salaam. Mwanamuziki Khadija Mnoga (Kimobitel) wiki iliyopita alitambulishwa rasmi kwa waandishi wa Habari kujiunga na Bendi ya Extra Bongo akitokea bendi ya African Stars (Twanga Pepeta) aliyoifanyia kazi kwa miezi kadhaa. Juzi Ijumaa na Jana Jumamosi ndiyo zilikuwa siku rasmi za kutambulishwa kwa mashabiki na wapenzi wa extra Bongo.

Kimobitel akiimba na Mkurugenzi wa Extra Bongo Ally Choki wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la "Mgeni" ndani ya New White house wakati wa utambulisho wake rasmi.
Comredi Ally Choki aka Mzee wa Farasi
Kimobitel akizikonga nyoyo za mashabiki wake ndani ya Meeda Sinza usiku wa kuamkia leo wakati aliokuwa akitambulishwa rasmi kwa mashabiki wa maeneo ya Sinza na maeneo ya jirani.
Makamanda wa Extra Bongo wakiongozwa na Ally Choki mwenye Tsheti nyeupe mbele, kutoka kushoto ni Banza Stoni, Kimobitel na mwisho kulia ni Rogert Hega aka Katapila wakiimba wimbo mpya wa Hadija Mnoga aka Kimobitel.
Ally Choki Mkurugenzi wa Extra Bongo akiimba kwa furaha wimbo wa "Mgeni" ulotungwa na Khadija Mnoga (Kimobitel). 
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo SPORTS - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template