Headlines News :
Home » » YANGA YATAMBA KUIKABILI SIMBA MZIMA MZIMA LEO

YANGA YATAMBA KUIKABILI SIMBA MZIMA MZIMA LEO

Written By Bashir Nkoromo on Wednesday, October 3, 2012 | 5:07 AM

Kocha mkuu wa Mabingwa wa klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, timu ya Young Africans Sports Club Mholanzi Ernie Brandts amesema kikosi chake kipo tayari kuikabili timu ya Simba sc katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom hapo kesho uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. 

Akiongea na mtandao wa klabu www.youngafricans.co.tz. leo asubuhi katika mazoezi ya mwisho yaliyofanyika shule ya sekondari Loyola, amesema wachezaji wake wote wapo safi, wana ari ya mchezo na ushindi, hivyo anaamini mchezaji yoyote atakayempanga atafanya vizuri.

Yanga mabingwa watetezi wa kombe la Kagame mara mbili mfululizo, wataingia uwanjani kusaka point 3 muhimu ambazo zitaipelekea kusogea katika nafasi nzuri ya kutwaa Ubingwa msimu wa 2012/2013.

Katika mazoezi yaliyofanyika leo asubuhi, kocha Brandts aliweza kuwatumia wachezaji wote waliosajiliwa katika msimu huu wa ligi, isipokuwa Salum Telela pekee ndio mchezaji majeruhi .

Kocha Brandts amesema amefurahi kwa wachezaji wake wote kuwa fit, kiakili, kimwili na kifikra kwa ajili ya mchezo wa kesho, na hivyo anawaahid wapenzi na wanachama wa Yanga wajitokeze kwa wingi kuona soka safi na la kuvutia.

Mchezo utaanza majira ya saa 1 jioni kwa saa za Afrika Mashariki na utaonyeshwa moja kwa moja dunia nzima  na kituo cha runinga cha Supersport cha nchini Afrika Kusini.

'MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI YOUNG AFRICANS'

'DAIMA MBELE NYUMA MWIKO': CHANZO:www.youngafricans.co.tz

Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Google+ Followers

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo Blog: SPORTS PAGE - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template