Headlines News :
Home » » TFF YAPONGEZA KWA UONGOZI MPYA TRFA

TFF YAPONGEZA KWA UONGOZI MPYA TRFA

Written By Bashir Nkoromo on Sunday, November 4, 2012 | 8:27 PM


DAR ES SALAAM, TANZANIA.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa uongozi mpya wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tanga (TRFA) uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika Novemba 3 mwaka huu.

Ushindi waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TRFA walivyo na imani kubwa kwao katika kusimamia mchezo huo mkoani Tanga.

TFF inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya TRFA ambayo imechaguliwa chini ya uenyekiti wa Said Soud.

Uongozi huo mpya una changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha unaendesha shughuli za mpira wa miguu Tanga kwa kuzingatia katiba ya TRFA pamoja na vyombo vya mpira wa miguu vilivyo juu yake.

Pia tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya TRFA na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuhakikisha uchaguzi huo unaendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF.

Viongozi waliochaguliwa ni Said Soud (Mwenyekiti), Beatrice Mgaya (Katibu), Khalid Mohamed (Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF) na Juma Mgunda (Mwakilishi wa Klabu TFF).
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Google+ Followers

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo Blog: SPORTS PAGE - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template