Headlines News :
Home » » MPAMBANO WA UBINGWA WA NGUMI KUFANYIKA MKWAKWANI TANGA

MPAMBANO WA UBINGWA WA NGUMI KUFANYIKA MKWAKWANI TANGA

Written By Bashir Nkoromo on Saturday, March 2, 2013 | 7:53 AM


MPambano la masumbwi kutetea makanda wa mabara wa WBF(world boxing forum) wategemea kufanyika katika uwanja wa mkwakwani jijini  Tanga kwa  kuwakutanisha  Alan Kamote, ambae ni bingwa mtetezi wa  mkanda huo aliouchukua  nchini Malawi  kwa  kuzipiga na  Jumanne Mohamed  wa tanga  ambae anavyo vigezo  na sifa zote  za kuugombania ubingwa huo.
Jumanne Mohamed ambae alipata nafasi  ya kugombania  ubingwa  wa dunia  nchini Namibia na kuipoteza kwa kupigwa na mnamibia  nafasi hiyo imejirudia tena,safari hii katika ubingwa wa mabara na kuugombania katika ardhi ya nchini mwake.
Muandaaji wa pambano hilo Ally Mwanzoa  akizungumza  na viongozi wa ngumi nchini pamoja na katibu mkuu wa ngumi za kulipwa  Ibrahim  kamwe amesema ameamua kuandaa pambano hilo ili Alan kamote autetee  mkanda wake alioupata  Blantaya nchini Malawi usije ukapoteza kwa kutokuutetea ubingwa wake huo, na kukaa na uongozi wa ngumi  kwa kuangalia bondia gani  anafaa  na ikaamuliwa  jumanne Mohamed anafaa kutokana na sifa alizonazo na upinzani walionao  mabondia hao utaleta mshawasha na msisimko mkoani Tanga, kwa hiyo haina haja ya kumleta mtu kutoka nje ya nchi.mwanzoa aliendelea  kwa kusema pia kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi  kati jj ngotiko  na  haji juma wa Tanga katika pambano la raund kumi, na kutakuwepo na mapambno mengine mengi y a utangulizi.ALAN KAMOTE AKIWA NA MIKANDA YAKE.jpg

Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo SPORTS - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template