Headlines News :
Home » » BONDIA IDDY MKWERA AMGALAGAZA LUCAS NDULA MUHEZA TANGA

BONDIA IDDY MKWERA AMGALAGAZA LUCAS NDULA MUHEZA TANGA

Written By Bashir Nkoromo on Monday, April 1, 2013 | 12:55 AM

Bondia Iddy Mkwera akinyooshwa mkono juu baada ya kumgalagaza Lucas Ndula wakati wa mpambano wa mabondia wa Dar na Muheza Mkwera alishinda kwa pointi mpambano hou wa raundi sita uliotahalishwa kwa ajili ya kuinua mchezo wa ngumi Wilaya ya Muheza  na kusherekea sikukuu ya Pasaka
Bondia Iddy Mkwela wa Dar es salaam kushoto akimshambulia vikali mpinzani wake Lucas Ndula wakati wa mchezo wao uliofanyika katika uwanja wa jitegemee Muheza Mkoa wa Tanga Mkwera alishinda kwa point
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' akiwa na mabondia wake walipotua katika wilaya ya Muheza Mkoani Tanga kwa ajili ya kwenda kuamasisha mchezo wa masumbwi katikati ni Iddy Nkwera na Martin Richard wote kutoka Dar es Salaam
Kocha wa mchezo wa ngumi Kimataifa Rajabu Mhamila 'Super D' wa tatu kushoto akiwa na mabondia Iddy Mkwera na Martn Richard baada ya kushuka katika gari kwa ajili ya kuhamasisha mchezo wa masumbwi Wilaya ya Muheza wakati wa sikukuu ya Pasaka wakiwa na wapenzi wa mchezo huo katika stend kuu ya mabasi hayo
Mabondia walio shiriki katika mpambano huo wakiwa katika picha ya pamoja
Kocha wa mchezo wa Masumbwi Wilaya ya Muheza Charles Muhiru 'Spins' akiwa na mgeni rasmi ambaye amefanikisha kuandaa mpambano huo Allan Augastino akisalimiana na mabondia kutoka Dar.
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' wa tatu kulia akiwa na baadhi ya mabondia waliocheza ngumi katika uwanja wa jitegemee muheza
Mabondia wakiwa na Super D



Mabondia wa Kutoka Muheza wakionesha shoo ya masumbwi wakati wa kusherekea sikukuu ya Pasaka katika viwanja vya Jitegemee Muheza
Mabondia wa Kutoka Muheza wakionesha shoo ya masumbwi wakati wa kusherekea sikukuu ya Pasaka katika viwanja vya Jitegemee Muheza
Bondia George Allen akinyooshwa mkono juu baada ya kushinda mpambano huo
Bondia Lucas Ndula wa Muheza kushoto akioneshana uwezo wa kuoneshana uwezo wa kutupiana masumbwi na Iddy Mkwera wa Dar es salaam katika uwanja wa jitegemee muheza wakati wa sikukuu ya Pasaka Mkwera.
Baadhi ya Mashabiki waliojitokeza katika mpambano huo
Bondia Lucas Ndula wa Muheza kushoto akioneshana uwezo wa kuoneshana uwezo wa kutupiana masumbwi na Iddy Mkwera wa Dar es salaam katika uwanja wa jitegemee muheza wakati wa sikukuu ya Pasaka Mkwera.
Bondia Iddy Mkwera akinyooshwa mkono juu baada ya kumgalagaza Lucas Ndula wakati wa mpambano wa mabondia wa Dar na Muheza Mkwera alishinda kwa pointi mpambano hou wa raundi sita uliotahalishwa kwa ajili ya kuinua mchezo wa ngumi Wilaya ya Muheza  na kusherekea sikukuu ya Pasaka. PICHA ZOTE NA www.superdboxingcoach.blogspot.com

Na Mwandishi Wetu
Bondia Iddy Mkwera wa Dar es salaam ameibuka mshindi baada ya kumgalagaza bondia Lucass Ndula wa Muheza wakati wa mpambano wa kuhamasisha masumbwi Wilayani Muheza uliochezwa wakati wa sikuku ya Pasaka katika uwanja wa Jitegemee

Mpambano ulioanza kwa ndula kuanza kwa kasi na kushangiliwa na wapenzi wengi katika raundi ya kwanza na ya pili upepo ulianza kumbadilikia raundi ya tatu baada ya kukata pumzi uku akitupa ngumi bila mpangilio wakati Mkwera akipanga mashambulizi na kupiga ngumi kali za kushitukiza zilizo mfanya Ndula kutulia

Raundi ya tano ilikuwa ni mfululizo wa makonde yaliyorushwa na Mkwera kwa ajili ya kumuhadhibu ndula ilipofika raundi ya sita na ya mwisho wa mchenzo ndula alipigwa upcat ambayo ilimchanganya na kufanya kuwa nje ya mchezo kwa kushika magoti

ambapo aliokolewa na kengele iliyoashilia kumaliza mpambano huo wa raundi sita na kufanya Iddy Mkwera kuibuka na ushindi wa point akipeperusha vema bendera ya Dar es salaam katika wilaya ya Muheza 

Mfadhili wa mpambano huo ambaye aliwezesha kila kitu ikiwemo kupereka mabondia kutoka Dar pamoja na ulingo maarumu kwa ajili ya masumbwi  Allan Augastino ame haidi kurudia kufanya onesho hilo la wazi katika viwanja hivyo hivyo vya Jitegemee Muheza mkoa wa tanga wakati wa sikukuu ya Iddi na kuwataka wapenzi kujitokeza kwa wiki

Mpambano huo uliofanyika katika katika viwanja vya wazi vya Jitegemee iliwavuta wapenzi wengi wakiwemo watoto ,wanawake na vijana mbalimbali waliojitokeza kwa wingi
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo SPORTS - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template