Mama wa Mitindo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fabak Fashions na wandaaji wa onyesho la Lady in Red, Bi. Asia Idarous Khamsin akizungumza na wadau tasnia ya mitindo waliojumuika kwenye After Party ya kuwashukuru wadau waliotoa michango mbalimbali tangu kuanza kwa onyesho la Lady in Red nchini Tanzania.
...Ally Rehmtulla, Martin Kadinda watunukiwa vyeti vya mafanikio
Na Andrew Chale
HALFA maalumu ya kilele cha Miaka 10 ya onesho la mavazi la ‘Lady in Red Super Brand’ usiku wa Jumamosi Februari 22, lilikuwa la aina yake kwa kuvutia watu mbali mbali ndani ya Ukumbi na mgahawa wa kisasa wa Nyumbani Lounge, ambapo pia wadau walikabidhiwa vyeti.
Tukio hilo la aina yake ambalo lilivuta umati mkubwa wakiwemo wadau wa ubunifu na mitindo nchini pamoja na watu maalufu, Pia walipata kupita kwenye zuria jekundu (red carpet) na kupata picha za ukumbusho wa tukio hilo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Fabak Fashions na wandaaji wa onyesho hilo kila mwaka, Asia Idarous Khamsin, aliwashukuru wadau waliojitokeza kwenye halfa hiyo maalumu na kutoa vyeti kwa watu na taasisi zilizoweza kuliunga mkono onyesho hilo pamoja.
Mama wa Mitindo Bi. Asia Idarous Khamsin akipozi wakati wa zoezi la kugawa vyeti na models waliovaa mavazi yaliyoonyeshwa kwenye onyesho la kutimiza miaka 10 la Lady in Red lililofanyika hivi karibuni.
“Tunamshukuru Mungu kwa kufikisha Miaka 10 ya Lady in red, hadi kufikia hapa, tumeweza kufanya mambo makubwa katika tasnia hii ya ubunifu wa mavazi na jukwaa hili litaendelea kuwa chachu ya mafanikio zaidi na zaidi” alisema Asia Idarous.
Na kuongeza kuwa, jukwaa hilo ndilo pekee lililoweza kuibua wabunifu wakubwa hapa nchini huku wengine wakipeperusha vyema bendera ya Tanzania nje ya nchi, wabunifu hao ni pamoja na Ally Rehmtullah, Martin Kadinda, Ahmed Abdul, Faustin Simon.
Mwanamitindo wa siku nyingi Fiderine Iranga akipokea cheti kutoka kwa Mama wa mitindo Asia Idarous Khamsin kwa kutambua mchango wake katika tasnia ya mitindo nchini.
Wengine ambao nao wanachipukia kwa sasa akiwemo Salim Ally, Salim Ally, Abdul Mwene,Baby Julieth, Baby Masai na wengine wengi.
Asia Idarous alibainisha kuwa, wapo mbioni kuliboresha jukwaa hilo na kuwa la Kimataifa ikiwemo kushirikisha wabunifu wa kimataifa na kufungua milango kwa wabunifu wa ndani kujiuza kimataifa.
Mwanamitindo mkongwe Fiderine Iranga akimkabidhi zawadi Mama wa Mitindo Bi. Asia Idarous kwenye After party ya kuwashukuru wadau waliofanikisha sherehe za kutumiza miaka 10 ya onyesho la Lady in Red iliyofanyika mwishoni mwa juma kwenye kiota cha Nyumbani Lounge jijini Dar.
Aidha, katika halfa hiyo pia wageni na wadau waliofika walipata kushuhudia shoo fupi ya mavazi yaliyobuniwa na Lucy Warere wa Tifu tifu fashions, Beda Masai na Asia Idarous Khamsini.
Asia Idarous aliwataja wadhamini waliodhamini halfa hiyo ni pamoja na Times fm, Michuzi media group, MOblog, DTV, Nyumbani Lounge, Darling air, G one Media, Channel Ten, CTN na wengine wengi.
Mbunifu wa Mavazi nchini Ally Rehmtullah akipokea cheti cha shukrani ya ushiriki wa onesho la Lady in Red kutoka kwa Mama yake Mlezi Asia Idarous Khamsin.
Cake ya After Party ya Onesho la Lady in Red iliyoandaliwa maalum kwa kuwashukuru wadau mbalimbali waliofanikisha sherehe za miaka 10 ya Lady in Red nchini.
Honest Arroy wa 360 Degrees akikata cake kwa niaba ya wadau kwenye After Party ya Lady in Red iliyofanyika mwishoni mwa juma kwenye kiota cha Nyumbani Lounge.
Model Richard akililishwa kipande cha cake na Mama wa Mitindo Asia Idarous Khamsin kama shukrani ya kushiriki maonyesho mbalimbali ya Lady in Red.
Wadau mbalimbali waliojitokeza kwenye After Party ya kusheherekea miaka 10 ya Lady in Red wakitazama matukio mbalimbali kwenye luninga ndani ya kiota cha Nyumbani Lounge.
Mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima, Andrew Chale akilishwa kipande cha cake na mmoja wa Models kwenye After Party ya kuwashukuru wadau waliofanikisha tangu kuanzishwa onesho la Lady in Red mpaka leo hii kutimiza miaka 10 kwenye tasnia ya mitindo nchini.
Wadau wakiwa wamepozi kwenye kiota cha Nyumbani Lounge wakati wa After Party ya Lady in Red iliyofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar.
Mdau akipata Ukodak na Models.
Mama wa Mitindo nchini Asia Idarous Khamsin akipata ukodak na mwanamitindo Mustafa Hassanali kwenye After Party ya kuwashukuru wadau walioshiriki kwenye onesho la Lady in Red lililotimiza miaka 10 hivi karibuni.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !