Bondia Habasi Hamisi wa Kigoma akikwepa konde la Mustafa Murinho wakati wa mashindano ya Nelson Mandela Open Championship yaliyofanyika katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es salaam Morinho alishinda kwa point mpambano huo na kuingia fainal
|
Bondia Finias Genga kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Haruna Swanga wakati wa mashindano ya Nelson Mandela Openchampion ship yaliyofanyika katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es salaam Swanga alishinda kwa TKO ya raundi ya kwanza na kufanikiwa kuingia fainal ya mashindano hayo Picha Nawww.superdboxingcoach. |
Bondia Haruna Swanga akinyooshwa mkono juu kuashilia ushindi wake |
Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis akisaidia kufunga mlingoti wa taa katika mashindano hayo |
Aisha Vonialis |
Na Mwandishi Wetu Kawe
Mjumbe wa maendeleo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis amesema wanawake wanatakiwa wawe na msukumo mkubwa katika kuhakikisha wanajitokeza kwenye mchezo wa masumbwi
akizungumza wakati wa mashindano ya kumuenzi Rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini Nelson Mandela Open Boxing Championship yaliyofanyika katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es salaam
Mjumbe huyo alitoa wito kuwa wanawake wanaweza hivyo wajitokeze katika kucheza mchezo wa ngumi na kuangalia mchezo huo kama michezo mingine akitolea mfano unaona katika mashindano haya wanawake ndio walio ongoza kuja kwa wingi kwa kuwa wanapenda mchezo siku zote tulizo kuwepo hapa katika viwanja hivi wanawake wanakuja kushingilia sana tu
aliongeza kwa kusema kuwa wanaomba mashilika,makampuni tasisi mbalimbali pamoja na watu binafsi kuja kusaidia mchezo wa masumbwi upate wadhamini wa kutosha kwani mashindano hayo yamekutanisha mikoa mbalimbali nchini kwa sasa hivyo wadau wote wanaombwa kujitokeza kudhamini mchezo huo
katika mashindano hayo ya kuingia fainali bondia Mustafa Morinho alimsambalatisha Abbasi Hamisi uku Jonson Swanga akimpiga Disson Everest na Abuu Said akimdunda Frank Msindo na Haruna Swanga akimwazibu bila huluma bondia Finias Genga kwa TKO ya raundi ya kwanza
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !