Headlines News :
Home » » MAZISHI YA MCHEZAJI WA ZAMANI NA MMOJA WA WAANZILISHI WA TIMU YA MAJI MAJI YA SONGEA

MAZISHI YA MCHEZAJI WA ZAMANI NA MMOJA WA WAANZILISHI WA TIMU YA MAJI MAJI YA SONGEA

Written By Bashir Nkoromo on Monday, March 3, 2014 | 10:45 PM

Mzee Abdala Alli alikuwa mmoja wa waanzilishi wa timu ya Majimaji ya Songea wana lizombe, yeye na wenzake watatu ndiyo walianzisha timu hiyo, Alikuwa mzee Mbegambega, Mzee Mshamu wakiongozwa na Mhe, Laurensi Mtazama Gama hao wote kwa sasa ni marehemu.
PICHA NA MPENDA MVULA.
 Mmoja wa watani wa Kabila la Wayao akimpaka unga usoni mtoto wa Kwanza wa kiume Hamisi Abdala Alli,
 Siyo Igizo ni utani kati ya Wamwela na Wayao.
 Mfiwa uruusiwi kufuta huo unga ukifuta tu wanakuja na debe zima wanakumwagia bora uwe mpole.
 Mzee Abdala Alli muda wake mwingi aliutumia kwenye mchezo wa mpira mpaka tatizo la upofu lilipompata ndipo akastaafu mambo ya soka akawa mshauri tu kwa Viongozi wa timu yake ya Majimaji.

 Mwili wa Marehemu ukitoka ndani ya nyumba yake.

 Watu wengi walijitokeza.

 Watani wa Kiyao wakishangilia.
 Watani wa Kiyao wakimfuatisha marehemu alivyokuwa akitembea enzi ya Uhai wake.
 Amezikwa kwenye Mashamba yake hapa Kipera Songea.

 HAPA NDIYO MWISHO WA SAFARI YAKE
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Google+ Followers

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo Blog: SPORTS PAGE - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template