Katibu
wa STDFAA, Jafari Makatu akizungumza
na waandishi wa habari leo
Jijini Dar es Salaam,
Kulia ni Mwenyekiti wa STFFAA, Ali Baucha na
kushoto ni Mdhamini
wa Chama hicho,
Ahmed Olotu.
|
Chama cha Waigizaji wa filam mkoa wa Kinondoni (STDFAA) wamemuomba Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kuhimiza kukamilishwa Sera ya filamu ili ianze kutumika kuwasaidia wasanii katika mambo mbalimbali hususani ya kisheria.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu wa Chama hicho, Jafari Makatu alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kwa ajili ya kutoa pongezi kwa Serikali ya Awamu ya Tano pamoja na kuzungumzia changamoto zinazowakabili katika tasnia ya filamu nchini.
Makatu amesema kuwa Sheria ya Filamu ni muhimu katika tasnia hiyo hivyo ikiharakishwa itasaidia wadau wa tasnia hiyo kufanya kazi kwa uwazi na usalama wa hali ya juu kwa kuwa watakua wanalindwa na sheria.
“Tunamuomba Waziri wetu Mhe. Nape atuharakishie Sera ya Filamu kwa sababu sheria hiyo itatusaidia kuoanisha mambo mbalimbali ya kisheria kuanzia kwenye uandaaji wa kazi zetu hivyo, kupelekea kufanya kazi kwa ufanisi na kutoa kazi bora zaidi”. Alisema Makatu.
Ameongeza kuwa sheria hiyo pia itawasaidia katika suala zima la Haki miliki na Haki shiriki, malipo stahiki kwa kila kazi, masoko, madaraja ya waigizaji na wadau wote wa tasnia ya filamu pamoja na ulazima wa kila msanii kujiunga katika vyama husika vitakavyowasaidia katika mambo mbalimbali.
Aidha, Katibu huyo ameiomba Serikali kuwekeza kwenye sanaa ili kuwawezesha kuifanya kazi hiyo kwa ufanisi na kuchangia katika Pato la Taifa pia amemuomba Mhe.Nape kuwatafutia eneo maalum la ardhi ambalo litawasaidia katika kufanyia shuhuli zao za kurekodi filamu.
Ametoa rai kwa wasanii kujiunga katika vyama mbalimbali vinavyowahusu ili kuleta umoja, mshikamano na tija katika kazi za sanaa,amesisitiza wasanii kujiunga na Bima za Afya.
Naye Mdhamini wa Chama hicho, Ahmed Olotu amewaomba waandishi wa habari kutumia kalamu zao katika kuwasaidia wasanii kupambana na wauzaji wa filamu feki kwa kuwa wanarudisha nyuma maendeleo ya wasanii na kupunguza pato la Taifa.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !