Afisa Masoko wa PSPF, Magira Werema, (kushoto), akimkabidhi sehemu ya vifaa hivyo, Mkuu wa Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Ukonga jijini
Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange Bakari.
NA
K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
MFUKO
wa Pensheni wa PSPF, umekabidhi vifaa vya michezo kwa wanamichezo wa Jeshi la
Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam na kasha kufuatiwa na PSPF bonanza la michezo ya mpira wa miguu, mpira wa pete, Ngumi na
Judo.
Akikabidhi
vifaa hivyo vya michezo Agosti 25, 2016, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko
huo, Abdul Njaidi, alisema, PSPF imeamua kutoa vifaa hivyo ili kuunga mkono juhudi
za serikali katika kuinua michezo nchini.
“Nyinyi
mkiwa kama sehemu kubwa ya wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, tunayo
furaha kutoa vifaa hivi vya michezo kwani baada ya kutekeleza majukumu mazito
ya kitaifa mnahitaji kushiriki michezo ili kujenga afya lakini pia kuinua
vipaji vyenu,” alisema na kuongeza,
“Nichukue fursa hii kuwahamasisha mjiunge na
PSPF kwani kuna faida nyingi mtapata kutokana na kutoa mafao mbalimbali yatakayoboresha
maisha yenu kama ambavyo kauli mbiu yetu inavyosema, PSPF ni chaguo lako sahihi
na kamwe hutajutia uamuzi wako wa kujiunga na Mfuko huu.” Alisisitiza Njaidi.
Akipokea
vifaa hivyo kwa niaba ya wanamichezo hao, Mkuu wa Kikosi Maalum cha
Magereza-Ukonga, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange Bakari,
aliishukuru PSPF kwa msaada huo wa vifaa vya michezo kwani vitawawezesha
wanamichezo hao kushiriki michezo katika mazingira bora ya kiuanamichezo.
Baada
ya makabidhiano hayo, wanamichezo hao walionyesha uwezo wao katika michezo ya
mpira wa miguu, ngumi, mpira wa pete, na judo.
Afisa Matekelezo (Compliance), wa PSPF, George Mnasizu, (kushoto), akigawa vipeperushi vyenye maelezo ya kina ya huduma zitolewazo na Mfuko huo kwa baadhi ya wanamichezo wa Jeshi la Magereza
Njaidi akiwa na Mkuu wa Kikosi hicho, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Kikosi Maalum cha Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam, Rajabu Nyange Bakari, na wacheza judo wa kikosi hicho wakiwa katika picha ya pamoja na vipeperushi vya PSPF.
Njaidi akimkabidhi sehemu ya vifaa hicho, Nahodha wa timu ya mpira wa pete (Netball), wa timu ya Magereza Ukonga, Pili Enzi
Werema akimkabidhi sehemu ya vifaa hivyo kocha wa soka wa timu ya Magereza, Sajenti Hassan Mulego
Njaidi akikagua timu ya soka ya Magereza Ukonga, ambayo ilimenyana na Kikosi Maalum cha Magereza Dar es Salaam, wakati wa bonanza hilo la michezo
Soka likiendelea baina ya Kikosi Maalum na timu ya MagerezaSoka likiendelea baina ya Kikosi Maalum na timu ya Magereza
Soka likiendelea baina ya Kikosi Maalum na timu ya Magereza
Hizi ndio Gloves na flana zilizotolewa kwa wana masumbwi (ngumi)
Pambano la masumbwi likiendelea
Pambano la masumbwi likiendelea
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi, akiwa na Mkuu wa Kikosi Maalum cha Magereza jijini Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange Bakari, wakati akitoa nasaha kwa wanamichezo kabla ya kuanza kwa bonanza hilo
Nasaha za mgeni rasmi kwa wanamichezo
Wanamichezo wakishangilia hotuba
Onyesho la Judo
Werema akimkabidhi sehemu ya vifaa hivyo vya michezo, Kocha na Afisa Michezo wa Kikosi Maalum cha Magereza Dar es Salaam, Inspekta Francis Tabu
Soka likiendelea baina ya Kikosi Maalum na timu ya Magereza
<!--[if gte mso 9]> |
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !