Warembo wa Miss Ilala 2016 wakiwa katika picha ya pamoja.
**************
SHINDANO la Kumsaka Miss Ilala 2016 linafanyika
leo katika ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency – Kilimanjaro, jijini Dar es
Salaam.
Mbali na kufanyika kwa shindano hilo pia
litatumika kuadhimisha miaka 20 ya shindano la Miss Ilala tangu kuanza
kufanyika kwake na warembo mbalimbali waliowahi kushiriki na kushinda taji hilo
watahudhuria.
Mratibu wa shindano hilo, Erick Othman kutoka
Kampuni ya Gogetime Enterprises ya jijini Dar es Salaam, alisema kuwa warembo
14 watapanda jukwaani kuwania taji hilo pamoja na tiketi ya kushiriki shindano
la Kitaifa la Miss Tanzania 2016 linalotaraji kufanyika baadae mwaka huu.
Othman alisema mgeni rasmi katika shindano hilo
leo hii ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, huku burudani ikitolewa na
wasanii mbalimbali akiwepo Rubby.
Amewataja warembo wanaoshindana kuwania taji
hilo kuwa ni Osmunda Mbeyela, Mercy Zephania, Melody Tryphone, Dalena David,
Nuru Kondo, Julitha Kabete, Sporah Luhende, Queen Nazil, Lilian Omolo, Mariam
Maabad, Brenda Allan, Sabrina Halifa, Agriphina Nathaniel na Grace Malikita.
Kwa upande wa zawadi za washindi, Kitundu
alisema kuwa mshindi wa kwanza atajinyakulia kitita cha sh milioni moja pamoja
na portable TV kutoka Startimes, huku mshindi wa pili akipata sh 700,000 na
kingamuzi, na mshindi wa tatu akipata sh 300,000 na kingamuzi pia.
Alisema kuwa mshindi wan ne atapata sh 200,000
na watano atapata sh 150,000 pamoja na kingamuzi huku warembo wengine watapata
kifuta jasho cha sh 50,000.
Kiingilio katika shindano hilo ni Sh 50,000
kawaida na Sh 100,000 kwa viti maalum (VIP).
Wadhamini ni Coca cola, Atsko, Darling, Channel
10, Kitwe General Traders, Uefa Goo, Mustafa Hassanali, Majira, High Spirit,
StarTimes, Father Kidevu Blog na wengineo.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !